KAMUSOKO ANAWASUBIRI KWA HAMU WAETHIOPIA JIONI
Kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko amewapia wapinzani wao Wolayta Dicha wa Ethiopia katika mchezo wao wa leo kwa kusema wamejiandaa vilivyo kuwafunga.
Yanga leo Jumamosi inacheza na Dicha katika mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa. Kamusoko raia wa Zimbabwe na wachezaji wenzake wamepania kuifunga Dicha katika mchezo huu wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho.
Kama Yanga itaitoa Dicha na kutinga makundi kwenye michuano hiyo, itakuwa ni mara ya pili ndani ya misimu mitatu kwani katika msimu wa 2015/16, timu hiyo iliishia kwenye hatua hiyo.
Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo wa leo, Kamusoko alisema: “Michuano ya Caf ukiangalia ni migumu na ina mazingira magumu sana ya kusonga mbele kutokana na jinsi ilivyo.
“Ukiangalia kwa hatua hii tuliyofikia timu ikicheza mechi mbili na kushinda basi inaingia makundi, kitu hicho usichukulie rahisi, unatakiwa kufanya kazi kweli.
“Sisi tumejiandaa vizuri na tunawajua wapinzani wetu wapo vipi, tunajipanga kufanya vizuri kuhakikisha tunaingia tena hatua ya makundi.
“Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuisapoti timu yao kwa sababu wasipoisapoti itakuwa ngumu kwetu kufanya vizuri kwani tunajiona kama tunachokifanya si kizuri na hakiwapendezi wao mashabiki.”
CHANZO: CHAMPIONI

No comments