UNYAMA Jijini Mwanza: Bibi Amchoma Visu Vya Moto Mjukuu Wake Akimtuhumu Kupoteza Peni Ya Sh. 200
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia bibi mmoja ajulikanaye kwa majina ya Laurencia Athanas mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini Mwanza kwa tuhuma za kumchoma visu vya moto mjukuu wake na kumsababishia majereha mbalimbali mwilini akimtuhumu kupoteza peni ya sh. 200.
Mtoto huyo aitwaye Jackson Hosea ( 10 ) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kiseke iliyoko Ilemela Jijini Mwanza alifanyiwa unyama huo nyumbani kwa bibi huyo ambaye ni mzazi wa mama yake aishiye Nzega siku ya Ijumaa jioni tarehe 23 May 2015.
No comments