BINTI NUSURA ABAKWE, AKATWA MAPANGA..MUONE ALIVYOJERUHIWA YANI
Elizabeth Sombe anayedaiwa kunusurika kubakwa. Akizungumza na Amani juzi, Elizabeth alisema aliamua kuja Dar kufanya kazi baada ya kukatisha masomo yake akiwa darasa la sita kutokana na ugonjwa wa kifafa na hali duni waliyonayo nyumbani kwao.“Siku moja nyumbani alikuja rafiki yangu na kumwambia mama yangu kuwa amenitafutia kazi Dar hivyo nijiandae kuondoka naye. Nilijiandaa, nikaja Dar.
Jeraha alilolipata baada ya kujeruhiwa na panga. “Siku ya tukio, ilikuwa Jumatatu ya wiki iliyopita usiku nakumbuka, bosi wangu alinituma dukani kununua vocha usiku kama saa tatu hivi ndiyo nikavamiwa na vijana wanne, wakanifunga kitambaa usoni na kuanza kunivua nguo, nilijitahidi sana kupiga mayowe kuomba msaada kwa watu wa jirani na wao walipoona napiga mayowe wakaanza kunicharanga mapanga mpaka nikapoteza fahamu. Nilipokuja kuzinduka nilijikuta niko hapa hospitali asubuhi, sikujua nilifikaje,” alisema Elizabeth.
Aliendelea: “Sina msaada wowote ule kwani hata kurudi Mbagala naogopa na sitaki kumuona yule mama machoni mwangu maana sijamuona, naomba wasamaria wema wanisaidie kwani mpaka sasa sijui nikitoka nitakwenda wapi kwani tangu nimekuja Dar ni miezi miwili tu hata mshahara sijawahi kulipwa.
Jeraha la mguuni. “Nahitaji msaada wa nauli na mavazi kwa kuwa sina nguo na hata zile nilizokuwa nimezivaa siku ile zilikuwa zimechanika zote, bora nirudi nyumbani nikamsaidie mama kwani nilimuacha akiwa mgonjwa na sijui anaendeleaje maana ana ujauzito uliopilitiza miezi na alikuwa mbioni kufanyiwa operesheni.”
Kwa yeyote aliyeguswa kumsaidia binti huyo ili aweze kurejea kwao Iringa, anaweza kutuma pesa kwa namba 0712 121330.A
KHAA! Binti aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Sombe (13), mkazi wa Mafinga mkoani Iringa ambaye alikuja jijini Dar kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wodi ya Mwaisela namba mbili, Dar baada ya kucharangwa mapanga na kundi la vijana kufuatia kukataa kubakwa.
“Nilipokelewa na rafiki wa yule mama Neema ambaye anaishi huku, akanipeleka kwa mtoto wake anaitwa mama Junior. Ni Mbagala Rangi Tatu lakini naye anaishi maeneo hayohayo.“Nilianza kufanya kazi ikiwemo kumlea mtoto, kufua, kufanya usafi wa ndani na kupika lakini siku nyingine chakula cha mchana alikuwa akimtuma mtu atuletee nyumbani,” alisema Elizabeth. Jeraha alilolipata baada ya kujeruhiwa na panga. “Siku ya tukio, ilikuwa Jumatatu ya wiki iliyopita usiku nakumbuka, bosi wangu alinituma dukani kununua vocha usiku kama saa tatu hivi ndiyo nikavamiwa na vijana wanne, wakanifunga kitambaa usoni na kuanza kunivua nguo, nilijitahidi sana kupiga mayowe kuomba msaada kwa watu wa jirani na wao walipoona napiga mayowe wakaanza kunicharanga mapanga mpaka nikapoteza fahamu. Nilipokuja kuzinduka nilijikuta niko hapa hospitali asubuhi, sikujua nilifikaje,” alisema Elizabeth.

No comments