Breaking News

Boko haram wachoma vijiji na kuuwa watu 37.>>>>

 Wanachama wa kundi la vijana wanaofanya kazi za sungu sungu   huko kaskazini  mwa Nigeria wanasema kundi la wanamgambo la Boko haram wamechoma vijiji 6 na kuuwa watu 37 katika shambulizi jipya karibu na eneo la ngome kubwa ya waasi hao katika msitu wa Sambisa.

Vikosi vya vijana hao wanaoiunga mkono serikali viliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba mashambulizi yalitokea Jumatano usiku.Gazeti la taifa la Nigeria liliripoti kwamba vijiji vyote katika jimbo la Borno,vilikuwa Koshifa , Matangle , 

Buraltuma,Darmanti, Almeri  na Burmari.
Mmoja wa askari sungu sungu hao Ahmed Ajimi aliliambia shirika la AP kwamba waathirika walikuwa wakulima ambao hivi karibuni walirudi vijijini kwao baada ya askari wa Nigeria kuwaondoa Boko haram katika maeneo mapema mwaka jana.

No comments