Changamoto aliyonayo Wema katika siasa ni kuwabadilisha watu jinsi wanavyomfikiria -Meneja
Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema anaamini kuwa muigizaji huyo anaweza kuwa kiongozi mzuri japo changamoto inayomkabili ni kubadilisha mawazo ya watu juu yake hasa kutokana na maisha yake ya ustaa na mapenzi.
Martin ameiambia Mpekuzi kuwa kinachotakiwa sasa ni kuwabadili watu waanze kumchukulia kama mwanamke anayeweza kuwa kiongozi.
“Watu wengi wametokea kumsupport kwa sababu walikuwa wanamsikia baba yake akimtaka aingie kwenye siasa, na wengine walikuwa wanamtaka Wema aingie kwenye siasa,”amesema Martin.
“Lakini ana kazi kubwa ya kuweza kubadilisha watu jinsi wanavyomchukulia. Kwahiyo anachukulia positive kwa sababu watu aliokuwa nao wameweza kumsupport. Lakini kabla hatujafika huko sasa tutamuona kama kiongozi sioo kama msichana wa bongo movie. Tumuamini Wema kama anaweza kuonyesha tu nia hata asipopata tukumbuke kuonyesha nia tu ni kupata, kwa sababu ana ndoto kubwa sana anataka kuzifanya,” ameongeza.
Hivi karibuni Wema alitangaza nia ya kuwania ubunge wa viti maalum kwa tiketi cha chama cha mapinduzi mkoani Singida.
Kupitia Instagram aliandika:
Naanza kwa kusema Alhamdulillah kwa kufikia hapa nilipo na nawashkuru sana wazazi wangu kwa kunileta duniani na kunilea katika maadili mazuri… Nawashkuru pia kwa kunipa Elimu na kunipa chochote nilichokitaka but more over kwa kunipa support kubwa katika uamuzi wowote niliokuwa nimeufanya… Kwanzia kushiriki Miss Tanzania mpaka pale nilipoamua kujiingiza katika maswala ya sanaa.
Vitabu vya dini vimeandika inapaswa tumshukuru Mungu kwa kila jambo, liwe zuri au baya… Pale Mungu alipoamua kumchukua Daddy Sepetu wangu niliumia sana na nikawa nimeona kama maisha yangu yalirudi nyuma kidogo, maana ilinibidi nianze kuishi maisha ya No More Daddy Sepetu….
Maana nilikuwaga ni kipenzi cha Daddy wangu cuz I happen to be da last born, mwenyewe alikuwa akiniita Miss World wake…. Nakumbukaga My Late Daddy Sepetu alishawahi kuniambia kuwa nijaribu kujiingiza katika politics since yeye na siasa ilikuwa ni kama uji na mgonjwa… And I remember nilimwambia ,”Daddy Sepetu NO sitoweza” …
Alikuwa heart broken sana maana alihisi nikijaribu ntaweza na kilichokuja kumvunja moyo ni nilipochukua uamuzi wa kufanya International Business na sio hata Political science au chochote kilichohusu Siasa nilipoenda Chuo
But hakukata tamaa… Akazidi kuniambia naweza na nilizidi kukataa… Daddy Sepetu wangu This is for u…. Leo hii nimejikuta mwenyewe nimefanya uamuzi mzito wa kujiingiza kwenye Siasa na kuona wat it has in store for me… Najua you are looking down on me smiling… Ila tu jua kuwa Your wife ambaye ni my Darling Mother nae pia amechangia kiasi kikubwa sana…
Nawapenda sana wazazi wangu maana wanajua Whats Best for me… Haya sasa naingia vitani… Na sitokubali Defeat… Tho kuna mengi yanaweza tokea… Namkabidhi Allah yote…. Na niko tayari kwa chochote… Penye nia siku zote njia haiwezi kukosekana.
No comments