Breaking News

EX- WA DIAMOND PLATINUMZ, PENNY AJITABIRIA KUWA MCHUNGAJI!

Imelda Mtema
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amejitabiria kuwa huenda siku za baadaye akawa mchungaji maana amekuwa akitabiri mambo flani kisha yanatokea.
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’. Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Penny alisema kwenye Tuzo za Watu zilizotolewa juzikati alipata maono kuwa Wema Sepetu na Millard Ayo watapata tuzo na kweli siku ya tukio ikawa hivyo.
“Unajua mimi nakaribia kuwa mchungaji, nimekuwa nikipata maono mengi ambayo hatimaye hutokea. Ni kitu ambacho baadhi wanaweza kuona utani lakini naamini siku moja inaweza kuwa hivyo,” alisema Penny

No comments