Breaking News

Gongo ilichukua headlines nyingi toka Rombo, kuna hii imetokea India pia



Hivi karibuni ishu ya wanaume wa Rombo kujihusisha na pombe haramu aina ya gongo na kusahau majukumu ya familia zao ilikaa kwenye headlines kwa muda mrefu na hata kufikia kuzungumzwa sana hata bungeni
 
Matumizi ya unywaji wa pombe hiyo si tu inanyweka Tanzania kwani leo headlines zimehamia nchini India baada ya watu 35 kupoteza maisha katika mji wa Mumbai baada ya kunywa pombe hiyo na wengine kulazwa hospitali.
 
Hata hivyo Serikali ya nchi hiyo imeingilia kati baada ya kutaka uchunguzi wa kina ufanyike huku watu watatu wakishikilia kwa tuhuma hizo.
 
Unywaji wa pombe hiyo umeshika kasi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo huku bei ya kununua imekua iko chini ya dola moja na kufanya idadi ya wanywaji kuomgezeka huku Mwaka 2011 kuliripotiwa kupoteza maisha kwa watu 170 kutokana na unywaji wa pombe hiyo.

No comments