Breaking News

Mwili wa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba Kusafirishwa Kesho Kwenda Mkoani Shinyanga Kwa Taratibu za Mazishi>>SOMA HAPA



MWILI wa  Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unataraji kusafirishwa kesho Jumanne Juni 16, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum, amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu, viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.

Amesema marehemu amefikwa na umauti huo, baada ya kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP)  pamoja na Figo.

Hata hivyo amesema kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.

Salum amesema marehem anatarajiwa kuzikwa Alhamis mkoani mkoani Shinyanga .

 Sehemu ya wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu  Mufti Alhaj Sheikh Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo.
Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akibadilishana mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa walipofika nyumbani kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B leo jijini Dar es Salaam
Kulia ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.

No comments