Breaking News

Ray J Kutumia Dola 30 Kwa Ajili Ya Birthday Ya Mbwa Wake>>



“I hit it first” hit maker Ray J, mwenye umri wa miaka 34, anampenda mbwa kwa kiasi ambacho ameamua kumfanyia sherehe maalum kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa, sherehe ambayo itafanyika Petrock Hotel and Spa iliyopo Encino, California, ambapo wageni watapita kwenye red carpet kabla ya kuingia.

Taarifa za TMZ zimeeleza, chakula kwa wageni, pia kutakuwa na sehemu maalum kwa ajili ya chakula cha mbwa na keki maalum kwa ajili ya mbwa wake anayeitwa Boogotti na marafiki zake watakuwa hapo.

Lakimi, mtu mmoja hatokuwepo ambae ni Princess Love, ambae alikuwa akimmiliki mbwa huyo mpenzi wa zamani wa Ray J.

Star wa “The Love and Hip Hop” waliachana vibaya mwezi Oktoba kitu kilichopelekea Princess kuondoka na mbwa wao watatu, kitu ambacho kimefanya Boogotti abaki peke yake.
 
Haiko wazi kama mbwa wa Princess watahudhuria birthday bash ya Boogotti.

No comments