SIKU CECH ALIPONUSURIKA KIFO: ILIKUA NI ‘SAVE’ YA MAISHA YANGU>>
“Ilikua ni save kubwa zaidi kufanya katika maisha yangu” ni maneno ya golikipa Peter Cech akisimulia siku aliponusurika kufa na kushindwa kuendelea na mechi.
Golikipa Peter Cech anajua lugha nne, ni msomi wa masomo ya historia na saikolojia, pia ndio golikipa ghari zaidi katika historia ya Barclays Premier League.
Pamoja na yote, kinachoshangaza zaidi ni namna alivyoweza kurudi tena uwanjani na kuendelea kudaka pamoja na majeruhi yale ya kichwa.
Katika kona ya nyumba yake kuna kadi, barua, vipeperushi na jezi za sio tu mashabiki wa Chelsea ila wachezaji kutoka timu pinzani walionesha sapoti yao siku ambayo hakuna mtu alijua Peter Cech angepona.
“Nimetunza kila kitu. Ni kumbukumbu muhimu katika maisha yangu. Nawashukuru kwa dua zenu, sintosahau” anasema Cech
Cech ambaye aliumia kichwa Oktoba 2006, anazungumza kiingereza na kireno vizuri sana. Ukiacha lugha ya nyumbani kwa Jamhuri ya Czech, pia anajifunza kihispania.
Tukio la kuumia kwa Cech lilitokea katika mechi dhidi ya Reading mwezi Oktoba 14, 2006 walipokuwa wanawania mpira na mchezaji Stephen Hunt. Hakua na fahamu na ilikua ni siku ya simanzi kwa wanamichezo wote duniani.
Ilitangazwa kwamba Cech asingeweza kucheza tena katika maisha yake lakini, yeye mwenyewe anasema, “nilitaka kuonesha utofauti ingawa ilikuwa ni ngumu sana kwa wakati huo. Nilipata shida hata kuongea”.
Katika hali ya kushangaza, Cech alianza mazoezi mepesi huku akiwa na program ya miezi 4 ya kuwa sawa. Alipitia magumu mengi lakini hatimaye, januari 2007 akarudi tena uwanjani, safari hii akivaa Helmet (kofia ngumu). Cech anasema kofia hiyo inamsaidia kujihisi salama zaidi.
Cech alikuwa na mahusiano mazuri sana na kocha Jose Mourinho. Hata siku anarudi tena kazini Januari 20, 2007, kocha Jose Mourinho alimsema kama ni usajili mpya wa paun 50m.
Hiyo ndiyo ‘save’ ya muda wote ya maisha ya golikipa huyo anayejiunga Arsenal.
Kashinda kila kitu na Chelsea ni zaidi ya neema kwa washika bunduki wa London.
No comments