Roma akamilisha Usajiri BASATA
Msanii Roma Mkatoliki ametimiza masharti aliyopewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kumtaka ajisajili Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kuwa akifanya hivyo atakuwa ametambulika na kuwa huru kufanya kazi.
Roma Mkatoliki jana April 5, 2018 amekwenda Baraza la Sanaa la Taifa na kujisajili kama ambavyo aliagizwa na viongozi wa serikali na kusema kuanzia leo atakuwa huru kufanya kazi na sasa anarudi rasmi katika muziki.
Mar 1, 2018 Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki alifungiwa kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharau wito wa BASATA na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Msanii huyo ametumikia kifungo hicho kwa mwezi mmoja na siku tano hivyo kifungo chake kimeisha jana baada ya kujisajili BASATA.
Msanii Roma Mkatoliki ajisajili na kukabidhiwa rasmi cheti cha kutambulika na Baraza la sanaa la Taifa jana April 05 2018, Hii ni baada ya kupewa sharti na Wizara ya Habari ya kujisajili kwanza Basata ili aondolewe adhabu yake ya kufungiwa miezi 6.
No comments