#Uzinduzi: Bilioni 5 Zimetuumika Kujenga Ukuta Madini ya Tanzanite
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Martin Busungu amesema gharama za ujenzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite, ni Sh5 bilioni.
Jenerali Busungu amesema ukuta huo wenye kilometa 24.4 utazunguka eneo lote la mgodi wa Tanzanite na tathmini ya awali, ilionyesha kwa kilometa 21 zingetumika Sh 4 bilioni.
Akizungumza leo Aprili 6 katika uzinduzi wa ukuta huo, Busungu amesema vikosi 20 vya JKT vimejenga ukuta huo.
“Tumetekeleza kwa uadilifu na uamnifu ujenzi huu. Tunatoa shukran za dhati kwa taasisi za uhandisi Tanzania kwa ushirikiano wao,” amesema
Amesema Jeshi la JKT lipo tayari kutekeleza maaagizo yoyote yakatayotolewa kwa mustakabali wa Taifa.
“Hata hivyo kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwamo ugumu wa ujenzi hasa katika miamba, uwepo njia za nyingi za maji ambazo hata hivyo wahandisi wa Pangani River walisaidia,” amesema
Leo Rais John Magufuli anazindua ukuta huo. Viongozi mbalimbali, wakuu wa mikoa, wa wilaya na mawaziri wamehudhuria hafla hiyo.
No comments