Breaking News

CHADEMA Yabaini Kituo Hewa cha BVR Geita



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa  Geita  kimesema kimebaini   kwa kituo hewa cha kujiandikisha wananchi  kwenye daftari la wapiga kura kiitwacho Buharahara “B”   katika kata mpya Bomba Mbili.

Hayo yalisemwa na  Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Geita,  Nguru Tanganyika, alipozungumza na waandishi wa habari.
 
Alisema Chadema haikitambui  kituo hicho ambacho kipo   kinyume na makubaliano yaliyokuwapo kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Magareth Nakainga  na vyama vyote vya siasa.

Tanganyika alisema  wamekibaini kituo hicho hewa kutokana na jitihada za viongozi wa chama hicho kutembelea vituo mbalimbali  vya kujiandikishia.
 
“Ofisi ya Chadema wilaya ya Geita kama mdau wa uchaguzi,  imebaini kituo hewa cha Kata ya Bomba mbili kinyume na makubaliano kati ya Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi wa Mji wa Geita na  vyama vya siasa.
 
“Tulikubaliana  hakutakuwa na uandikishaji wa wapiga kura Kata ya Bomba mbili kwa kuwa haijakidhi vigezo vya sheria kufanya uchaguzi kwa sababu ya kukosa  wakazi wanaotosheleza kupiga kura.

No comments