Breaking News

Wafanyabiashara Waonywa Kupanda bei Mwezi Mtukufu



MWENYEKITI wa soko kuu la Majengo mkoani Dodoma,Godson Rugazama amewataka wafanyabiashara kutokupandishia bei ya bidhaa katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Rugazama alitoa wito huo jana,alipokuwa akitoa taarifa ya mapato na matumizi katika mkutano mkuu wa umoja wa wafanyabiashara wa soko kuu la Majengo.
 
Rugazama aliwataka wafanyabiashara kuutumia mwezi huo kutafuta dhawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu na kuacha kupandisha bei kiholela.

‘’Niwatakie mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, nawaomba wafanyabiashara wenzangu kuutumia mwezi huu kwa kutafuta amali na tuache kupandisha bei kiholela hasa za futari’’
 
‘’Ila kwa kupitia umoja wetu tutahakikisha bei hazipandi kiholela kwa kuwasaidia kupata mahitaji yao wale wanaofunga,pia tunawakaribisha kuja kununua bidhaa katika soko letu’’alisemaLugazama.

Kwa upande wake, Naibu Katibu wa soko hilo, Iddi Vumba alisema wanakabiliwa na changangamoto ya kuchakaa kwa miundombinu mbalimbali ikiwemo Paa la Soko,mifereji ya maji taka na korongo lililopo katika eneo  hilo.
 
Alisema  changamoto wanayokabilianayo ni kusumbuliwa na askari  nyakati za usiku, wakati wanaposhusha mizigo nje ya soko hilo, hivyo kumtaka mkurugenzi kuingilia suala hilo ambalo limekuwa ni kero kwa wafanyabiashara.
 
“Kuna wafanyabiashara husuasani akina mama ambao hushusha mizigo yao usiku nje ya soko kutokana na taratibu zilizopo za kutoruhusu kuingiza bidhaa usiku,
 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manipaa ya Dodoma, Boniphace Micheal  alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16, soko hilo litapata fursa ya kukarabatiwa ili kuondokana na changamoto zilizopo.
 
Michaeli ambaye ni Ofisa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa manispaa hiyo,alisema kuwa kwa upande wao wanatambua changamoto zilizopo ikiwa kwa wafanyabiashara wenyewe na wadau wanaotumia soko hilo.
 
“Naomba niwahakikishie kuwa ikifika mwaka mpya wa fedha wa julai soko hilo tutafanya mabadiliko kulingana na mapato,ukizingatia kuwa soko la majengo linaongoza kwa ukusanyaji wa mapato ndani ya manispaa”alisema.

No comments