Breaking News

Rais Magufuli kuzindua ukuta mgodi wa Tanzanite leo

Rais John Magufuli leo Ijumaa Aprili 6, 2018 anazindua ukuta unaozunguka mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.

Kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli aliyoyatoa Septemba 2017 na kuliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kujenga ukuta ndani ya kipindi cha miezi sita.

Jana, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Ramadhan Dogoli amesema ujenzi huo umekamilika na leo kiongozi mkuu huyo wa nchi atazindua.

No comments